IMF Yaionya Afrika Mikopo ya Maliasili

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), #KristalinaGeorgieva ameeleza kusaidia wito wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao unaomba nchi za Afrika kubadili mkondo wa kuweka maliasili ya nchi kama dhamana katika mikataba ya mikopo.

Kwa upande mwingine, Rais wa #AfDB, Dkt. #AkinwumiAdesina ameonya kuwa endelea na utaratibu huo kutaweka mzigo mkubwa, kwani mikopo inayounganishwa na maliasili haina uwazi, ni ghali, na inaweza kufanya kulipa mikopo kuwa ngumu.

Kulingana na #BenkiYaDunia (WB), Afrika ina jumla ya mikopo 30 inayohusisha rasilimali (RBLs), ambapo wakopeshaji 13 wametambuliwa. Benki za #China zinadai asilimia 76 (Tsh. Trilioni 90.36) ya mikopo inayohusisha rasilimali za nchi barani Afrika, na Eximbank na CDB wako mstari wa mbele katika kutoa mikopo ya aina hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *