Bodi ya Utalii Ilivyomkana Kumtuma Mwijaku Ufaransa

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekanusha madai ya kumtuma mtangazaji na mwigizaji, Mwemba Burtony, maarufu kama Mwijaku, nchini Ufaransa kutangaza utalii kama balozi wa utalii kwa niaba ya au kwa gharama za Serikali.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na TTB, mwaka huu walishirikiana na Sekta Binafsi katika maonyesho ya utalii ya Ufaransa yaliyofanyika kuanzia Oktoba 03 hadi 05, 2023. Katika hafla hiyo, TTB ilikuwa na kampuni 12, ikiwemo kampuni ya Asha Tours EK. Kampuni hii ndiyo iliyomlipia Mwijaku kwenda Ufaransa kufanya utangazaji wa biashara yake inayohusiana na utalii, na kampuni hiyo ina makao makuu huko Hamburg, Ujerumani.

TTB imesisitiza kuwa hawakumtuma Mwijaku na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehusika na shughuli za utalii bila kufuata sheria na taratibu zilizowekwa nchini Tanzania.

Bodi ya Utalii imeongeza wito kwa watu wote kuzingatia sheria na taratibu katika shughuli zao za utangazaji na uhamasishaji wa utalii, ndani na nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *