Putin Ailaumu Marekani Mzozo Israel – Palestina

 

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati uliosababishwa na uvamizi wa ghafla wa kundi la Hamas la wapiganaji wa Kipalestina nchini Israel kusini wiki iliyopita ni uthibitisho wa uwezo mdogo wa Washington wa kutatua mizozo.

“Ninaamini wengi watanikubalia kwamba hii ni mfano wazi wa kushindwa kwa sera za Mashariki ya Kati za Marekani. Walijaribu kuudhibiti utatuzi wa amani, lakini kwa bahati mbaya hawakutilia maanani kutafuta makubaliano yanayokubalika kwa pande zote,” kiongozi wa Urusi alisema Jumanne.

Badala yake, Washington iliwatia shinikizo pande zote katika jaribio la kuwawekea suluhisho lake, aliongeza. Marekani “hawakutilia maanani maslahi ya msingi ya watu wa Kipalestina,” Putin alidai. Maslahi hayo kwa kiasi kikubwa yanajumuisha uundwaji wa taifa huru la Wapalestina, kama ilivyoainishwa katika azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, alibainisha.

Putin alitoa kauli hizo wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed al-Sudani, huko Moscow. Rais wa Urusi alisema anaamini mataifa hayo mawili yanakusudia kupunguza madhara yanayosababishwa na pande zote katika mzozo wa Israeli na Wapalestina kwa raia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *