Samia: Upole Si ujinga

Zanzibar, Septemba 1, 2023 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameapisha mawaziri na viongozi wengine katika sherehe iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo. Hatua hii inafuata uteuzi wa mawaziri uliofanywa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan aliwataka viongozi hao wateule kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia wananchi wa Tanzania kwa uaminifu na kujitolea. Alisema, “Sisi ni Watumishi wa Watu, mahusiano ni jambo zuri sana. Ukijipandisha unataka kukaribia Mbinguni hautatumikia watu, upole si ujinga.”

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pia alisisitiza umuhimu wa viongozi kuwa wawajibikaji na kuendeleza mabadiliko chanya katika jamii. Aliwataka kufanya kazi kwa kujituma ili kuinua maisha ya wananchi na kusaidia katika kuleta maendeleo endelevu ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *