Serikali Yaamuru Uchunguzi wa Vifaa Vinavyodaiwa Kupima Uwezo wa Akili

Serikali imechukua hatua kufuatia taarifa za Shule za Alfa za Jijini Dar es Salaam kutangaza matumizi ya Mashine za Anthropo-Biometric ambazo zinadaiwa kuwa na uwezo wa kubaini uwezo wa akili au vipaji vya wanafunzi.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Prof. Adolf Mkenda imetoa agizo la kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu vifaa hivyo. Profesa Mkenda amewataka wakaguzi wa elimu kujifunza kwa undani jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi katika kutambua utendaji wa ubongo wa wanafunzi. Aidha, ameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu ushirikiano wa wamiliki wa mfumo huo na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Tarehe 4 Machi 2023, Shule za Alfa ziliweka wazi Mfumo wa Kupima Vipaji ambapo ilielezwa kuwa mfumo huo unachukua vinasaba vya wanafunzi na taarifa hizo hutumwa Geneva kwa ajili ya uchakataji ili kuweza kubaini uwezo wa kila mwanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *