Msanii Haitham Afariki Dunia

Mwimbaji maarufu wa muziki wa Bongofleva, Haitham Kim, ambaye hivi karibuni kulianzishwa kampeni ya kuchangisha pesa kwa ajili ya matibabu yake, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Bwana Bryson, ambaye ni mume wa marehemu na ambaye AyoTV ilimkuta hospitalini juzi akiwa na AyoTV wakimsaidia kumuuguza Haitham, ameithibitishia AyoTV na MillardAyo kuwa Haitham amefariki leo Hospitalini hapo.

Katika mahojiano na @AyoTV_ siku za nyuma, Bryson alielezea jinsi hali ya Haitham ilivyobadilika ghafla siku saba zilizopita, akisumbuliwa na tatizo la kupumua. Awali, ilionekana kama homa ya kawaida, lakini baadaye hali yake ilizidi kuwa mbaya, na alilazimika kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua, pamoja na kuchomwa sindano za dawa kila siku, ambazo gharama yake ilikuwa kiasi cha shilingi laki saba kwa siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *