Mtanzania Atekwa Nigeria

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana, amethibitisha kuwa watu wasiojulikana nchini Nigeria wamemteka nyara Mtanzania ambaye ni Frateri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers), Melkiori Mahinini (27), ambaye ni Mzaliwa wa Parokia ya Kabanga Jimbo la Kigoma.

Tukio hilo lilitokea katika Jimbo la Minna nchini Nigeria tarehe 3 Agosti 2023, akiwa na mwenzake raia wa Burkina Faso, Padri Paul Sanogo. Watekaji wanadai kiasi cha Naira milioni 100 (Tsh. milioni 314.4) ili kuwaachia huru wote wawili.

Dkt. Bana aliongea na @AyoTV_ akisema kuwa tukio hilo ni kweli limetokea na kuongeza kuwa matukio ya utekaji nchini Nigeria sio jambo geni na mara nyingi watekaji hulenga kupata kikombozi (pesa) kwa kuwaachia mateka wao.

Ubalozi wa Tanzania unachukua suala hili kwa uzito na umuhimu mkubwa, na wanafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha maisha ya Mtanzania huyo na mwenzake wanakuwa salama na wanakombolewa haraka. Hata hivyo, Dkt. Bana aliwataka Watanzania kuwa makini na kuwa na umoja katika kushughulikia suala la utekaji nchini Nigeria kwani watekaji huwa wanaweza kusababisha madhara kwa mateka wao ikiwa kikombozi kitachelewa kutolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *