TANZIA: Babu Sikare Afariki Marekani

Msanii na Mwanaharakati wa kutetea haki za Watu wenye ulemavu wa ngozi, Babu Sikare maarufu Albino Fulani amefariki Dunia alfajiri ya leo February 08,2023.

Babu Sikare amefariki huko Columbus, Ohio nchini Marekani alipokuwa akiishi na kufanya shughuli zake za muziki.

Msanii Wakazi amesema “Amefariki Marekani alfajiri hii, alikuwa anaumwa, siwezi kuongea zaidi mpaka nipewe ruhusa na Familia na nisipopewa ruhusa siwezi kuongea cha ziada, ni Rafiki yangu wa karibu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu hali yake ilikuwa inaimarika halafu inaenda vibaya na kwa bahati mbaya amefariki”

Naye Mwanamitindo Flaviana Matata amesema “Nimetoa pole kama Rafiki, alikuwa Mtu mwema sana, kuongea na Vyombo vya Habari niachie Familia kuheshimu privacy yake kama Familia ndio wanaweza kuongelea”

Chanzo: Millard Ayo #Instagramupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *