Yanga Wakalipiwa Kuchanganya Nembo

 

Ebwana eh! Ukistaajabu ya mtandaoni utayakuta ya Yanga na nembo! Kwani hii imekaaje bwana..! Kwanza ruka na hii tweet hapa ilioandikwa na @AlfredSesei

Sasa ndio muweke logo ya CAFCL kwenye squad yenu inayoenda kushiriki CAFCC cup…mnapenda sifa za kijinga na hamna uwezo

Hili limetokeaje? Basi subiri nikupe mchapo. Siku ya jana Jumanne ya tarehe 07/02/2023 katika ukurasa rasmi wa Twitter wa Club ya Yanga walipost majina ya kikosi chao kitakachosafiri kwenda nchini Tunisia. Sasa kwenye post yao ambayo ilishafutwa tayari waliweka logo ya klabu bingwa ya CAF badala ya logo ya Shirikisho.

Na hili ndo likazua makasiriko. Jamani si kukosea tu logo na ujumbe umefika au kuna kingine jamani. Basi bwana hebu cheki hasira za wananchi zilivyovamia post hiyo iliyofutwa bwana…!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *