Matukio 5 Ya Kuhuzunisha Tetemeko la Ardhi Uturuki

Tetemeko la Ardhi lililozikumba nchi za Uturuki na Syria limeshika vichwa vya habari kote ulimwenguni kutokana na watu wengi kupoteza maisha na kuwapo kwa visa mbali mbali vya kuhuzunisha na kutoa machozi na vingine kutoa faraja baada ya tukio hilo.

Hapa nimekusogezea matukio ma 5 yaliyogusa watu wengi kwenye tukio hilo na shughuli nzima za uokoaji.

1. Mtoto aokolewa akinyonya kidole.

Katika hali ya kushangaza, mtoto mwenye umri wa miezi miwili ajulikanaye kama Mohammed Dogan Bostan, ameokolewa akiwa ananyonya kidole gumba.

Mtoto huyo, alipata majeraha machache tu na mama yake aliokolewa muda mfupi kabla ya uokoaji wa mtoto huyo.

2. Mtoto azaliwa chini ya kifusi

Katika hatua nyingine, Mtoto mchanga wa kike ameokolewa na waokoaji kutoka chini ya vifusi vya jengo kaskazini-magharibi mwa Syria ambalo liliharibiwa na tetemeko la ardhi siku ya Jumatatu.

Mama yake alipata uchungu punde tu baada ya janga hilo kutokea na akafanikiwa kujifungua kabla ya kufariki muda mfupi baadaye, ndugu zake wanasema.

Mtoto huyo kitovu chake kilikutwa kimeungana na mama yake aliyefariki. Baba yake, ndugu zake wanne na shangazi wamefariki katika janga hilo.

3. Baba na mtoto wake

Katika tukio lingine la kuumiza, baba pichani hapo juu, anashindwa kuachia mkono wa binti yake wa miaka 15 aliyekwishafariki na hajatolewa kwenye kifusi.

4. Binti wa Kisiria na mdogo wake

Moja la tukio lililowagusa wengi, ni la mtoto mdogo wa kike wa Syria kukutwa chini ya kifusi akimlinda mdogo wake, wote wameokolewa na wako salama.

Binti huyo ana umri wa miaka saba na amemlinda mdogo wake kama inavoonekana pichani hapo juu kwa takriban masaa 17.

5. Familia ya watu 7

Katika tukio jingine, familia ya watu saba waliokwama katika kifusi kwa takribani saa 40 wameokolewa bwote wakiwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *