TMA Yatoa Tahadhari Mvua Kubwa Leo Februari 9

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa  angalizo la mvua kubwa zinazoweza kuleta athari leo Februari 9 na kubainisha maeneo yatakayokumbwa na mvua hizo.

TMA imetaja maeneo hayo kuwa ni Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida, Lindi na Mtwara.

Athari zinazoweza kutokea kutokana na mvua hizo zimetajwa kuwa ni pamoja na maeneo kuzungukwa na maji, kuathirika kwa shughuli za kiuchumi na isafirishaji.

TMA imewataka wananchi kujiandaa na kuzingatiwa kwani kunatarajiwa kuwa na hali mbaya ya hewa katika kipindi cha siku tano.

Aidha, TMa imetaja mikoa mingine itakayokuwa na hali ya mawingu, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua kuwa ni Dar es salaam, Tabora, Kigoma na Katavi.

Kwingine ni Mikoa ya Pwani, ikijumuishwa na visiwa vya Mafia, Njombe Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Shinyanga Simiyu, Manyara, Tanga, kilimanjaro, Arusha pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwa ufafanuzi zaidi na viwango vya joto nchini tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *