Murkomen Akimbizwa Hospitali baada ya Kupata Jeraha

Senate Majority Leader Kipchumba Murkomen on the ground after being tackled in Kitui on Monday, September 16, 2019.

Kiongozi Mkuu wa Seneti na seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alilazimika kupelekwa hospitalini Jumatatu baada ya kupata jeraha wakati wa mchezo wa mpira wa miguu kati ya maseneta na wenzao wa MCA.

Seneta alichakuliwa na gari la wagonjwa na kupelekwa katika Hospitali ya Neema kwa matibabu.

Maseneta na MCA walikuwa wakicheza kwenye uwanja wa maonyesho wa Kitui wakati mpinzani alimgonga vibaya, na kumjeruhi.

Timu ya Seneti, iliyopewa jina la Bunge, ilipiga MCA 3-2.

Maseneta wapo Kitui kwa wiki kwa vikao vya kamati ambazo zitafanyika kaika kaunti ya Kitui. Hii ni sehemu ya mpango wa ‘Seneti Mashinani’.

Spika wa Seneti Ken Lusaka na Spika wa Kitui George Ndoto waliongoza uongozi wa mikutano yao katika mkutano wa mashauriano uliolenga ratiba ya wiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *