PICHA: Pesa sabuni ya roho! Mwimbaji wa Mihadarati ajipa raha pwani na vipusa

Image result for simple boy in mombasa

Maisha ya usanii kweli ni raha mustarehe na hivyo ndivyo msanii chipukizi wa Kibra Simple Boy ambaye amezua gumzo mtandaoni kupitia wimbo wake wa ‘Vijana tuache Mihadarati’.

Alizungumza kwenye mahojiano hivi majuzi na mcheshi Chipukeezy ambapo alisema kuwa watu wengi hawakutaka kujihusisha na mziki wake na pia muonekano wake.

Alikiri kuwa wengi wamemwita sura mbaya na ata baadhi yao kufikia kiwango cha kumpea jina nyani kwa muonekano wake.

Image result for simple boy and chipukeezy

Lakini yote yalikuwa mapito na sasa Stivo Simple Boy ni maarufu mitaani na jijini kupitia kwa wimbo wake wa Mihadarati.

Wikendi iliyopita, alikuwa anapunga upepo pale Mombasa na maisha yamebadilika kabisa kwake ata na akapata warembo kupindukia.

Stivo amepata kazi kupitia kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni ya Kupambana na Dawa za Kulewa (NACADA) kusaidia na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini baada ya kuhojiwa na Mkurugenzi Mtendaji Victor G. Okioma na mkurugenzi wa Bodi ya NACADA Vincent Muasia almaarufu Chipukeezy.

Hizi ni baadhi ya picha alizoziweka mtandaoni;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *