UTACHEKA: UTANI MITANDAONI JUU YA RASTAMAN KWENYE PICHA YA RAIS MAGUFULI

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akinunua samaki nakuwekewa kwenye kikapu siku ya jana kwenye soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam.

Siku ya jana Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alifanya matembezi kwenye soko kuu la samaki la Ferry jijini Dar es salaam na kuzungumza na wafanyabiashara sokoni hapo wale wa samaki na wale wenye biashara nyingine. Kitendo hiki kimepongezwa sana mtandaoni.

Huyu hapa traoreofficial_tz “Rais wa wanyonge, safi sana baba👏”

Katika moja picha inayotrend kwasasa mitandaoni ni ile ya ya Rais Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa kahawa na kwenye picha hiyo wako watu sita na watano akiwemo rais  wakikaa kwenye benchi pamoja na jamaa mmoja ambaye hakufahamika jina lake ila katambulika kwa kirahisi kwa kuwa na rasta pamoja na miwani mieusi.

Katika picha hiyo Rastaman huyo anaonekana kushikilia mfuko wa blue mapajani, hili limezua gumzo kubwa sana mitandaoni na haya hapa baadhi ya maoni ya wadau kutoka mtaandao wa instagram:

 

View this post on Instagram

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wauza kahawa katika eneo la Soko la Ferry ambapo aliagiza kuboreshwa kwa sehemu ya biashara hiyo kuanzia siku ya kesho.

Ameanza kuandika absolute_20  “ yeye anadai kila akiangalia picha hii anamuona rastaman pekee ” Hivi ni kwanini kila nikiangalia hii picha namuona Rasta peke’ke?”

Nae ramadhanseif042017 anaandika “Huyo rastafar pembeni ni ngumu nyeusi anaona wanamletea wenge kilingeni hahah” Kilingeni ni sehemu mahususi kwa vijana wengi kukutanika hasa mtaani na kufanya mambo mbalimbali kama kupiga stori za hapa na pale juu ya maisha na kupata viburudisho mbalimbali kam sigara n.k

Wengine nao wameandika juu ya mfuko alioubeba rastaman kama papaabm yeye anaandika “Rasta kama amepatwa na wasiwasi hv, ahaaaaa uzuri mfuko ndo elekezi upo mkonon kwake or kilichobebwa ndo ckijui” 

 

Kutokana na imani ya Rastafaris wengi juu ya mmea nae   tindigo_jr anaandika “Huyu rasta siyo bure anaweza akawa na ganja mfukoni.” 

 

Anaandika raj_hema79 “Rasta naona anapiga maombi awahi mzee kuondoka😂😂😂😂”

Wengine wakaaenda mbali zaidi kucoment juu ya raba aliyoivaaa mheshimiwa Rais kwa kufanania na ile aliyoonekana amevaa tarehe 24 mwezi wa tatu kwenye video iliyoonekana akishangilia na kuipongeza Taifa Stars kwa kuichapa Uganda 3 bila na kufuzu Afcon 2019, huyu hapa erry.popo

kaandika “Nimekumbuka hiyo DH chini siku TUNAWATOA WAGANDA”

Nawe pia unamaoni juu ya picha hii? Basi tuandikie hapo kwenye comment na usisahau kushare habari hii kwa rafiki zako!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *