Serikali:Watumishi wanaopatiwa vocha kutakiwa kutumia laini ya TTCL

IKIWA siku chache tangu Rais John Magufuli kutoa mwezi mmoja kwa ofisi yake na wizara mbalimbali kutumia huduma za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), leo serikali imeondoa sitofahamu na kueleza wanaotakiwa ni wale viongozi wanaopatiwa vocha.
Kadhalika, viongozi wa serikali ambao wameanza kuwatisha watumishi wa umma wametakiwa kuacha mara moja na kufuata agizo lililotolewa leo.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Mei 21 mwaka huu ikiwa ni muda mfupi baada ya kusomwa kwa majina ya ofisi zinazotumia mtandao wa mawasiliano ya TTCL, huku ofisi ya Rais ikiwa miongoni mwa zinazotumia mtandao huo.
Baaaa kutolewa kwa kauli hiyo ilizua mjadala katika mitandao ya kijamii na kuhoji iweje mtumishi wa umma kupangiwa kutumia laini ya TTCL wakati hayo ni matumizi binafsi ya mtu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas amesema hakuna agizo lililomlazimisha mfanyakazi wa seriklai kuwa na laini ya TTCL
Alisema msingi wa agizo hilo ni kwamba wapo viongozi ambao wanawekewa vocha na serikali, hivyo agizo hilo linawahusu wao na sio watumishi wote.
“Wale sasa wajitahidi angalau zile vocha zianze kuingia katika laini ya TTCL kama sehemu ya sisi kupenda cha nyumbani lakini hatujasema na wala hakuna hilo agizo la watumishi wote na viongozi ambao wameanza kuwatisha watumishi wa serikali hili ndio agizo,”
Aliongezea kuwa:”TTCL ni kampuni ambayo inafanya vizuri ni hiari ya mtu kujiunga ila kwa wale viongozi ambao wanapokea vocha watapewa kupitia TTCL ,” alisema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *