Museveni Aijibu Benki ya Dunian Juu ya Ushoga, Tutaongea Nao

Baada ya Benki ya Dunia kutangaza kusimamisha kutoa ufadhili na mikopo mpya iliyokuwa imeombwa na serikali kutokana na nchi hiyo kupitisha sheria inayopinga uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja, Rais Yoweri Museveni ametoa taarifa kuhusu suala hilo.

Museveni ameeleza, “Inasikitisha kuona Benki ya Dunia na watu wengine wanaotaka kutulazimisha kuacha imani yetu, utamaduni wetu, kanuni zetu, na uhuru wetu kwa ajili ya fedha. Hatuhitaji shinikizo kutoka kwa yeyote ili kujua jinsi ya kutatua matatizo yetu.”

Hata hivyo, kiongozi huyo amebainisha kuwa Uganda itaendelea kufanya mazungumzo na Benki ya Dunia ili kuangalia njia bora ya kutatua mkanganyiko uliopo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *