Polepole Atoa Onyo Kwa Wahuni

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey  Polepole amezitaja fursa mbalimbali zilizopo malawi na kuwaonya wahuni juu ya mienendo yao katika mambo mbali mbali.

Akizungumza katika mahojiano na Supa Breakfast ya East Africa Radio leo Februari 15 Balozi Polepole amesema ukitaka hela ya haraka basi Malawi ndiyo mpango mzima.

“Malawi ni kama kitovu cha bidhaa za Kitanzania. Kuna eneo linaitwa Tete hapa bidhaa za nguo kutoka Tanzania zinauzika sana na kama kuna sehemu unaweza kutengeneza dollar zako basi ni Tete. Watu wapeleke bidhaa na sisi kama Serikali tutatengeneza mazingira mazuri,”.Alisema Balozi Polepole

Kuhusu wahuni polepole alisema kuwa Zamani watanzania walikuwa wanaibiwa, mtu anakwenda kununua bidhaa kwa mtu usiyemjua. Lakini kwa sasa ubalozi umetengeneza orodha ambayo inatambulika na Serikali ya Malawi na Tanzania hivyo kama unataka soya utaambiwa muone flani kama ni mahindi muone flani.

”Mtu wa mwanzo aliyezungumza vizuri kuhusu wahuni ni Mwalimu Nyerere, kwahiyo mimi siwezi kuchukua sifa ya kuwa muasisi. Ila wahuni sio watu wazuri na hawafai kuchekewa na mtu yeyote na inatakiwa kauli ya taifa ya kukataa watu wahuni,” Alionya Polepole

Polepole aliongeza kuwa, hata katika mahusiano ya Tanzania na Malawi ole wake muhuni ajichomeke kwani atamfanya mambo siku atakuja kujuta.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *