Syria & Uturuki; Utafutaji wa Uokoaji Waingia Saa za Mwisho

 

Huku idadi ya waliofariki ikipita 35,000 katika nchi zote mbili, timu za utafutaji zinasema juhudi za uokoaji zinaingia katika saa zao za mwisho, huku kukiwa na matumaini madogo ya kuwapata wahasiriwa wakiwa hai chini ya vifusi baada ya zaidi ya wiki moja katika hali ya baridi kali.

Uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi la Jumatatu iliyopita utagharimu Türkiye pekee dola bilioni 84.1, kulingana na makadirio ya NGO moja ya Kituruki. Wakati huo huo, Qatar itatuma vibanda 10,000 na kreti zitakazotumika kama malazi ya muda kwenye Kombe la Dunia ili kuwahifadhi manusura.

Rais wa Syria Bashar al-Assad pia amekubali kufungua kwa muda vivuko viwili zaidi vya mpaka kutoka Türkiye ili kuruhusu mashirika ya misaada kuwafikia wale walioathirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *