Kamanda Murilo: Msiogope Kuomba Lifti Kwenye Difenda

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Murilo amewatoa hofu wananchi kuhusu kuomba lifti kwenye gari ya polisi  ‘difenda’.

Katika nukuu zilizosambaa katika mtandao wa kijamii wa twitter Kufuatia mahojiano ya Kamanda huyo katika kipindi cha Clouds 360 cha CloudsTV leo Februari 14, Murulo amefafanua suala hilo la lift kama inavyoandikwa hapa chini.

“Kuna mtu alishawahi kuomba lift kwenye Difenda hakupewa? Kwanini wanapanda watuhumiwa tu? Kwa mfano Difenda linakwenda Bunju, Tegeta, Kunduchu, Kitunda au Mwanagati, Kivule analiona kabisa limeandikwa Polisi na wewe unakwenda maeneo hayo kwanini usilisimamishe ukaomba lift?” Kamanda Murilo.

“Ishu ya kwamba ukiita Difenda unaambiwa ulipie mafuta hilo sio kweli ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi. Na hilo suala tumekuwa tukilisikia sana na tumekuwa tukilifuatilia sana lakini tukiwauliza wahusika (waliosema) nao wanasema na wao walisikia lakini hawana ushahidi” Kamanda Murilo.

Kama ilivyo ada, wadau nao wakafunguka maoni yao juu ya nukuu hiyo. Nini maoni yako mdau wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *