Polepole Afunguka Fursa Malawi

Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole amefunguka kuwa, malawi kuna fursa nyingi za kiuchumi za kuwanufaisha Watanzaniam

Akizungumza na Eatv Polepole amesema  Malawi mfuko wa saruji ni gharama mara mbili ya gharama ya Tanzania hivyo hiyo ni fursa kubwa sana na lengo ni kuisogeza Kariakoo karibu na mpaka wa Tanzania na Malawi na wanajipanga wilaya za Nyasa na Ileje ziwe wilaya za kiuchumi.

“Kwahiyo kwetu sisi kuna muingiliano mkubwa sana wa kibiashara na biashara inayovuka mipaka ambayo mwisho wa siku inanufaisha nchi zetu mbili, na inaenda sambamba na bidhaa mbalimbali za matumizi binafsi, bidhaa za viwandani na vipodozi,” amesema Balozi Polepole.

Polepole amewahakikishia Watanzania kuwa, Malawi ni kitovu cha biashara ambacho Tanzania ina maslahi makubwa sana kwa sababu bidhaa nyingi za watu wa kati na watu wa daraja la kawaida wanazipata kutoka Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *