Michael Joseph Kuendelea kushikilia kama Mkurugenzi mtendaji Safaricom, Msako wa Mridhi wa Bob Kuendelea

Safaricom interim CEO Michael Joseph.

Anayeshikilia kama Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom, Michael Joseph amesema ataendelea kukaa kwa muda zaidi kama anahitajika. Hii inakuja wakati bodi inafuatilia mpango wa kujaza pengo hilo.

Akiongea na wanahabari Ijumaa wakati wa mkutano wa telco, Joseph alisema wako kwenye hatua ya mwisho ya kuchagua mgombeaji wa nafasi hiyo ya juu.

“Nitakaa kwa muda mrefu kama ni lazima. Tulitumai tungekuwa na mwaka mwingine wa kutafuta mrithi tukijua kwamba Bob (marehemu) angejiondoa Agosti mwaka ujao, ”alisema.

Mipango ya kujiondoa kwa marehemu Bob Collymore kutoka kwa kampuni hiyo ya mawasiliano, ilitangazwa kwanza mnamo Aprili kutokana na sababu za kiafya.  lakini kutokana na kusisitiza kwa serikali kwamba anapaswa kuridhiwa na Mkenya kumechelewesha mpango huo.

“Bob alipofariki ghafla na bila kutarajia ilimaanisha kuwa tulilazimisha kuharakisha mpango huu,” Joseph alisema.

Mnamo Aprili, Reuters iliripoti kwamba bodi iliwahoji wagombea kadhaa kabla ya kumchagua raia wa kigeni  kutoka kwa kikundi cha Vodafone. Hata hivyo hawataja alikuwa ametoka taifa lipi.

Hata hivyo serikali ilipinga uteuzi huo kwa madai kuwa ilienda kinyume na makubaliano yalioafikiwa katika mkutano wa wanahisa mnamo 2017.

Uteuzi wa mtendaji mkuu katika Safaricom umebakai ni jukumu la Vodafone iliyoko Uingereza, ambayo ni mtendaji mkuu wa kampuni hiyo.

Hata hivyo, Ilihamisha uwezo huo hadi kwa Vodacom ya Afrika Kusini baada ya kubadilishana umiliki wa hisa mwaka wa 2017, ambayo ilibaki ikiwa na asilimia tano ya hisa, wakati kampuni ya Afrika Kusini ilibakia na asilimia 35 ya hisa.

Kutokana na mkataba huu muhula wa Bob uliongezwa hadi mwaka 2020.

Ingawa kampuni hiyo imekuwa wazi kuhusu mridhi, uvumi unaenea juu ya nani atakayejaza viatu vikubwa vya Bob. Baadhi ya majina yanayonong’onezwa ni ya Sateesh Kamath, afisa mkuu wa kifedha wa Safaricom.

Wengine ni pamoja na Sylvia Mulinge, afisa mkuu wa wateja wa Safaricom ambaye alikuwa ameteuliwa kuongoza Vodacom Tanzania kama Mkurugenzi Mtendaji lakini alikatazwa kibali cha kufanya kazi katika nchi hiyo.

Joseph Ogutu pia ameonekana kuwa na uwezo baada ya kusimama pahala pa Bob wakati alipokuwa katika likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *