Usifungulie Walaghai Mlango : Njia sita za kutambua Wasajili Halali wa Sensa

Serikali imesema iko tayari kufanya sensa ya sita ya kitaifa ya Kenya usiku wa Agosti 24, 2019. Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa ya Kenya imewaandika waandikishaji takriban 138,572, wasimamizi 22,268 na wasimamizi wa ICT 2,467  kwa zoezi hili.

Hii ni idadi kubwa ya wafanyikazi na haiwezekani Wakenya wote kujua majina na nyuso zao. Kuna wasiwasi kati ya Wakenya kutokana na zoezi hilo kufanyika usiku; Wengi wamedai kuwa wahalifu wanaweza kutumia fursa hiyo  ukikuzingatia watu wanatakiwa kuwafungulia waandikishaji milango yao.

Walakini, KNBS inasema vyombo vya usalama vinahusika kikamilifu na sehemu  ya kamati za sensa ya kitaifa na kaunti.

Image result for KNBS

Je, utawatambuaje waandikishaji halali wa KNBS?

1) Waandikishaji watakuwa na  Vitambulisho rasmi vya KNBS, sensa na nembo za serikali,zitakazo onyesha  majina yao na nambari ya vitambulisho vya Kitaifa.

2) Watavaa koti za rangi ya machungwa na ‘maroon’ kwa urahisi wa utambulisho.
Koti hizo zitakuwa zimechapishwa Kirauni na nembo za sensa upande wa mbele ya kulia na  kushoto mtawalia. Wito wa sensa ‘Jitokeze Uhesabike’ utachapishwa nyuma.

3) Watakuwa watu ambao unajua au umewahi kuwaona hapo awali. Kulingana na KNBS waandikishaji wamesajiliwa  wanakoishi na kwa hivyo wanajulikana na wenyeji.
Pia, wataambatana na wazee wa vijiji, viongozi wa vyama vya makazi na pengine, wasaidizi wa chifu.

4) Zoezi hilo ni bure na hakuna mtu anayepaswa kutoa malipo yoyote kwa waandikishaji.

5) Watarajie wawe na vidude vyeusi vya  Kompyuta (CAPI) vilivyo na nembo ya KNBS nyuma.
Hizi zitatumika kunasa data ya sensa kielektroniki.

6) Hawapaswi ‘kubisha’ zaidi ya mara moja.
Mara tu waandikishaji wakikamilisha kukusanya data kwa kila makao- mchakato ambao unatarajiwa kuchukua takriban dakika 30, kulingana na idadi ya watu waliopo-  viongozi wataandika nambari kwenye mlango au mahali pengine popote palipo wazi kuashiria kuwa hesabu imefanyika.

KNBS inawasihi wakenya wasifute nambari hiyo hadi muda wa zoezi likamilike.

Ni muhimu,  kutambua kuwa, kabla ya zoezi kuanza rasmi kutakuwa na mazoezi ya sensa ‘ambapo wakaazi na waandikishaji wataweza kujizoesha na zoezi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *