Sonko awataja viongozi serikalini waliowatelekeza ‘mpango wa kando’

Image result for mike sonko

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amewasha moto kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutangaza idadi kubwa ya viongozi maarufu wa serikali ambao huwachukua wasichana wadogo, kuwatia mimba, na kuwatupa. Aliapa kuwaweka wazi.

Sonko alisema kuwa amekuwa akipokea simu kutoka kwa wanawake kadhaa ambao walidai kuwa walizaa na viongozi wa juu wa serikali lakini wanajitahidi kulea watoto pekee yao.

Sonko alikuwa na haya ya kusema;

Baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka na kufanya uchunguzi wa wanawake sasa yanaonyesha kwamba makatibu 3 wa Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu 4, Magavana 7, Wagombea 2 wa Rais. wabunge 26, Maseneta 9, MCA 22 na wafanyibiashara maarufu 8 wamehusika katika kuwatia mimba wnawake na kukataa kuchukua majukumu ya watoto wao

Image result for mike sonko

Sonko aliendelea kusema kwamba ana ushahidi wa kutosha katika aina ya video, simu, mazungumzo ya WhatsApp, na ujumbe ambao atahakikisha wanawekwa kwenye magazeti kwa kila mtu kuona.

Sonko alisema kuwa ako tayari kuchapisha rekodi zote kwa majarida na kwa ukurasa wake wa Facebook na ata ikiwezekana chembechembe za DNA kupimwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *