‘Ilionekana kama hakujali,” Wahu azungumzia siku ya kwanza aligombana na Nameless

Image result for nameless and wahu

Wahu na Nameless ni miongoni mwa wanandoa ambao wanaheshimika sana nchini lakini kile ambacho wengi hawajui ni kwamba kama kila ndoa nyingine kumekuwa ni safari yenye changamoto.

Akizungumza kwenye hafla ya Samantha, Wahu aliweza kufichua jinsi siku ya kwanza waligombana na mume wake.

Kwa mujibu wa wa vyombo vya habari, Wahu alipoolewa, alitaka kubadilisha kila kitu kwa nyumba ya Nameless.

“Nyumba yangu ilikuwa imepambwa kabisa lakini yake ilikuwa na rangi nyngi ya nyeusi na kijivu tulipokuwa tunachumbiana. Nilikuwa nayo kwanza lakini tulipooana niliamua kujumuika naye kwake kwa sababu lilikuwa kubwa,” Wahu alisema.

Image result for nameless and wahu

Nameless kwa upande wake alijitetea akisema;

“Tulikuwa tumetoka harusi na nilichotaka ilikuwa mda mfupi nitulie lakini hangesikia ata kidogo. Alitaka kubadilisha kila kitu ikiwemo pazia. Alikuwa amekuja kwa hii nyumba kwa miaka nyingi kwa hivyo sikuelewa mbona alikuwa na haraka hivyo.”

Wahu hakujua ni kwa nini Nameless hakumsikia wala kumwelewa baada ya kubadilisha muonekano wa nyumba yao.

“Nilikuwa mwanamke wa kujitegemea na niliona kwamba alikuwa anatofautiana na mabadiliko yangu maanake nilibadilisha muonekana wa nyumba. Nilikuwa na hisia kuwa kama hawezi heshimu maamuzi yangu sijui kama ndoa yenyewe itakua.”

Yote tisa, wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka mingi na wamebarikiwa na wana wawili na wameendelea kuwa kielelezo njema kwa jamii na kwa vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *