Vera Sidika awasisimua wafuasi baada ya kumtambulisha mtanashati

Image result for vera sidika and bae

vera Sidika amewaacha wafuasi wengi vinywa wazi baada ya kuonyesha picha akiwa mweupe pepepe akiwa na mtanashati. Wafuasi wake wamepagawa na kushindwa kama wataangazia sura nyeusi ya vera ama mwanaume aliyemtambulisha.

Mbali na rangi yake ya sasa, baadhi ya wafuasi wameshangaa kama vera alimtema mpenzi wake wa siku ya mapenzi ya Valentines ama ni mambo ya kusisimua mtandao tu.

Mtangazaji Willis Raburu aliuliza, “Issa TBT or Restore factory settings?”

Image result for vera sidika and bae

Vera kwenye video zake za Instagramu, alielezea kuwa mwanaume huyo anamtunza kama mtoto mchanga.

“He treats me like a baby,”

Makampuni pia hayakuachwa nyuma, Bonfire iliuliza kama itawapeleka likizo.

“Honeymoons are holidays couples travel after wedding. Sijui ipangwe wapi?🔥🔥🔥. In-laws watoe maoni!,”

Itakumbukwa kuwa siku ya valentine, Vera Sidika alimtambulisha mwanaume mwengine baada ya kumtema msanii Otile Brown.

Wakati huo, Vera Sidika alikuwa marekani huku mpenzi wake akiwa mbali nae kilichomfanya kupigiana simu hadi usiku wa manane.

Je, huyu wa sasa anaweza kuwa mpenzi wa kweli ama ni kiki tu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *