Kauli ya Makonda kuhusu IST yaendeleza gumzo mitandaoni

Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, yazua utata katika mitandao ya kijamii baada ya kudai hawezi kumpatia mtu zawadi ya gari aina ya IST kwa kuwa gari hizo huongwa kwa watu mitaani.
Makonda aliitoa kauli hiyo jana katika tuzo za MO Simba zilizotolewa jijini Dar es Salaam ambapo alisema hawezi kumpatia mtu gari hizo ambazo zinahongwa.
“Kuna askari mmoja aliniuliza sasa mkuu tungetafuta kale kagari cha IST kanakula mafuta kidogo nikasema siwezi kumpa askari wangu gari ambayo mimi siwezi kuitumia zile wanahongwa hongwa watu huko mtaani,”alisema Makonda
Aliongezea kuwa:”Hata kama nakupa gari ndogo basi nikupe gari yenye hadhi kidogo unaweza kuipaki sehemu ukikaa nyuma ukafunga mkanda, sasa nitoe gari ambayo wanahongwa hongwa watu nimpe askari kweli? eti kweli askari uliyekula kiapo upewe gari ya watu,” alihoji.


Baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wameiponda kauli hiyo huku wakidai kuwa kauli hiyo ni ya uzalilishaji.
Robart Nchimbi alieleza kuwa Makonda amewavunjia heshima kwani watakuwa hata wanaogopa kuendesa gari hizo kutokana na kauli aliyoita.
“Huyu Makonda ana haribu biashara za watu na kama ana hela nyingi ni yeye atuache sisi tuendelee kutumia IST huyu sasa amelewa madaraka,”
Naye Peter Mrisho kupitia ukurasa wake aliandika kuwa huyu mdogo wetu kajisahau sana kwani huwa anatoa kauli za kuudhi watu.

 

https://twitter.com/Wakusnooz/status/1134404295875538944

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *