Naibu Waziri Aweso aangua kilio Pangani

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ameangua kilio mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kutatua kitendawili cha ujenzi wa barabara ya Tanga, Pangani, Bagamoyo kwa kiwango cha lami kama ujenzi huo upo au haupo.

Naibu Waziri Aweso amesema kuwa Wilaya ya Pangani ni kama imetengwa kwani ni muda mrefu sasa wamekuwa wakiomba lami lakini mar azote hupigwa kalenda ilhali wenzao wa wilaya nyingine kama Lushoto na Mkinga wameshapata lami.

Amesema watu wa Pangani wamekuwa wakisemwa kuwa hawapendi kazi badala yake hupendelea kukaa vibarazani na kupaka hina ilhali wanafanya kazi isipokuwa mazingira yao yamekuwa si mazuri.

“Tuna bahari, tuna mbuga ya Wanyama Sadani lakini bado tunashindwa kupata barabara ya lami licha ya vivutio vyote tulivyo navyo.”

Naye Waziri Kamwelwe amesema tayari ameshalifiksha suala hilo kwa Rais John Magufuli na tayari ameahidi kulifanyia kazi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *