Unashangaa Salamba kuomba viatu vya Banega? Ona hawa walivyomganda Gaucho

Mshambuliaji wa Simba Adam Salamba jana alionekana katika televisheni akiomba viatu kwa nahodha wa Éver Banega wa Sevilla ambapo kitendo hicho kimepokelewa kwa namna tofauti na mashabiki na wadau wa soka nchini, hasa wakikichukulia katika mrengo hasi.

Hilo limeonekana kama jambo geni na la ajabu, hili si jambo geni na hata kama lingekuwa ni jambo geni bado halina ajabu yoyote kwani ni sehemu ya mchezo ukizingatia wote walikuwa wakicheza uwanjani.

Ni jamba ambalo halitakiwi kuchukulwa wa wepesi kwani kwa mchezaji wa umri kama wa Salamba kucheza dhidi ya mchezaji kama Banega ni kitu kikubwa na historia katika maisha yake ya soka, kitendo cha kuomba viatu vya Banega baada ya game baadhi ya watu mitandaoni wamekipokea tofauti lakini ni kitendo cha kawaida na kimewahi kutokea katika soka mara kadhaa.

Wasifu wa Banega ni marudufu dhidi ya ule wa Salamba, kuanzia umri mpaka levo ya uchezaji. Banega amebakisha muda mfupi sana wa kucheza soka ukilinganisha na Salamba ambaye bado ana muda mrefu sana wa kucheza na kupata uzoefu mkubwa.

Mchezo wa jana kati ya Simba na Sevilla ni moja ya michezo yenye historia ya kipekee kwa Salamba na Simba na Tanzania kwa ujumla.

Kitendo cha Salamba kuomba kupata viatu kutoka kwa Banega ni sawa na mchezaji mwingine yeyote anapoomba kubadilishana jezi na mchezaji mwingine kwa sababu viatu pia ni sehemu ya sare muhimu kwa mchezaji kama ilivyo jezi.

Salamba alitaka kufanya hivyo walau kubaki na kumbukumbu kwake kuwa amewahi kucheza dhidi ya timu kubwa kama Sevilla na kuwa na Ushahidi kutokana na ukumbusho huo. Wengine wanahoji je, kama havimtoshi? Jibu ni kwamba viatu vile si kwaajili ya kuvaa ni kwaajili ya kubakisha kumbukumbu muhimu kwa mchezaji huyo na kizazi chake.

Ni kitu cha kawaida kwa wachezaji wengi duniani inapotokea anacheza na mchezaji wa kiwango cha juu au rafiki yake basi hubadilishana jezi kama kumbukumbu au ishara ya urafiki wao, mchezaji kama Banega inawezekana aliombwa na wachezaji wengi wa Simba jezi yake, hivyo Salamba akaona ili kubaki na kumbukumbu ya Banega aombe kiatu kama kumbukumbu.

Banega ana umri wa miaka kwa sasa, ana wasifu mkubwa amechezea timu ya taifa kubwa kama Argentina, kikosi kimoja na mchezaji bora mara tano wa dunia Lionel Messi na alikuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichoongozwa na Lionel Messi katika fainali za Kombe la dunia 2018 zilizochezwa Urusi, Banega amecheza timu kama Valencia, Atletico Madrid na Inter Milan vilabu ambavyo ni wachezaji wachache wa Afrika wamewahi kupata nafasi na ndoto ya wachezaji wengi duniani.

Wachezaji wa Raja Casablanca wakimvua Gaucho viatu

Tukio kama hili liliwahi kutokea 2013 nchini Morocco December 18 2013 katika mchezo wa club Bingwa dunia kati ya Atletico Mineiro ya Brazil iliyokuwa na Ronaldinho dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na mchezo kumalizika Atletico Mineiro ikifungwa 3-1, baada ya game wachezaji wa Raja Casablanca walivigombania viatu alivyokuwa amevaa Ronaldinho na jezi, yupo aliyechukua jezi na wengine wakagawana kiatu kimoja kimoja kama kumbukumbu kwao waliwahi kucheza dhidi ya Ronaldinho, sio kitu cha kawaida na nadra sana kupata nafasi ya kucheza dhidi ya wachezaji wenye heshima kubwa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *