Mashabiki wamcharukia Harmonize kutambulisha wimbo wake kwenye tukio la kufuturisha

 

Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watu mbalimbali maarufu na wasio maarufu, matajiri na wenye uwezo wa kawaida kufuturisha pale unapowadia mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wengi wao hufanya hivyo kwaajili ya kufanya sadaka na pengine kujiongezea thawabu au a’mali kwa Mungu kwa namna wanavyoamini kwa mujibu wa Imani yao.

Imezoeleka mara nyingi mahali panapoandaliwa Iftar basi huwa na mkusanyiko wa nyimbo zenye misingi na mahadhi ya Kiislamu (wengi hufahamu kama Qaswida).

 

Lakini hii imekuwa tofauti kidogo kwa upande wa Harmonize ambaye jana aliandaa hafla ndogo ya kufuturisha, hafla ambayo ilihudhuriwa na watu kadha wa kadha maarufu na wasio maarufu.

Katika hafla hiyo ya ufuturishaji Harmonize alitumia wasaa huo kutambulisha ngoma yake mpya ya ‘Never Give Up’ ambayo imeelezea simulizi ya changamoto ya Maisha yake ya muziki mpaka kufikia hatua aliyopo kwa sasa.

Hata hivyo hali hiyo imechukuliwa kwa mrengo hasi na baadhi ya watu ambao wamemkosoa kwa kunasibisha tukio la kufuturisha na pamoja na utambulisho wa wimbo wa kidunia.

Wamelaumu kwa usema msanii huyo amekwenda kinyume na misingi na maadili ya dini ya kiislamu kutokana na alichokifanya jana.

#trending #music

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *