Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameachiliwa huru.
Mahakama iliamuruu kwamba mbunge huyo alipe dhamana ya KSh 10 milioni ambazo zitatumika kwa matibabu ya masanii DJ Evolve ambaye mbunge huyo alimpiga risasi.
Aliamriwa kulipa pesa hizo vifungu vine huku malipo ya kwanza yakiwa kudhamini uhuru wake.
[VIDEO]: DJ Evolve's family opposes release of Embakasi East MP Babu Owino on bond; Babu's supporter arrested in court after shouting at State lawyer. pic.twitter.com/crA5IM5G3Y
— The African Voice (@teddyeugene) January 27, 2020
Vilevile ameonywa asitumie dawa zozote za kulevya ikiwemo pombe.
Familia ya DJ Evolve ilipinga kuachiliwa kwa mbunge huyo.
Babu Owino anapiganiwa na mawakili saba wakiwemo Cliff Ombeta na Dunstan Omari.