Kambi la injili humu nchini limekumbwa na kashfa nyingine ya ngono na udanganyifu, huku Mr. Seed akiwa mhusika mkuu.
Shabiki mmoja alitokea na kuonyesha jinsi baba wa mtoto mmoja alishiriki nae ngono kwenye makaazi yake ya Roysambu.
Kwa mujibu wa taarifa ya sauti iliyotolewa kati yake na msanii aliyesainiwa na Mr. Seed, Ndume, mwanadada huyo anakubali kuwa hajui mambo yangezidi unga kwa vile yeye alikwenda tu mahali pake akijaribu kupata ushauri jinsi ya kuendeleza kazi yake ya filamu.
Aliongezea kuwa Mr. Seed alimshawishi kushiriki naye ngono jambo ambalo hakuliona kama kubakwa.
Hali nzima imetoa taswira mbaya kwa mziki wa injili na cha kutia doa zaidi ni baada ya Ndume kukubali kumkumbuka na kumwambia asithubutu kutoboa hiyo siri.
Kwa namna fulani katika kashfa nzima, msanii wa injili Weezdom alijipata katikati mwa skendo hii kwa madai kuwa hawafahamiani vizuri na Mr. Seed na kinaweza kuwa ni chanzo cha kumharibia jina.
Kwa bahati mbaya, Weezdom hakushawishika na madai hayo na cha kushangaza ni kwamba alikuwa amekirekodi mahojiano yake na Mr. Seed sawia tu na ile ya Gavana Sonko.
Pia alionyesha kuwa tofauti kati yao iliyoonekana tu ilianza baada ya Weezdom alijaribu kuingilia kati na kumshauri Seed juu ya njia ya kufanya ili hiyo shida imwondokee.
“Kuna habari ambazo zinasambaa kwamba Mr. Seed alifanya kitendo cha ngono na mwanadada mmoja bila idhini yake na kama ndugu, nilimwambia ajue vile kushughulikia jambo hili kabla kuharibike jambo. Mr. Seed alikubali kwamba alimjua mwanadadalakini hakuishughulisha kumtafuta ili waongelee suala nzima. Baadaye alikuja kukabiliana na mimi lakini kwa bahati nzuri nilikuwa nimerekodi mahojiano yetu kwa namna ile tu wangesema nimewaharibia siri zao,” aliandika Weezdom.