MABADILIKO! Makamba Atupwa Mambo ya Nje, Tax Ulinzi Tena!

Januari Makamba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki . Hii ni hatua yenye athari kubwa katika tasnia ya sera za kimataifa na ushirikiano wa kikanda.

Makamba anachukua nafasi hii muhimu kutoka kwa Dkt. Stergomena Tax, Hii inathibitisha imani ya Rais Samia kwa Makamba na uwezo wake wa kuleta mabadiliko katika diplomasia ya Tanzania.

Awali, Makamba alikuwa akihudumu kama Waziri wa Nishati, na sasa ana nafasi mpya ya kusukuma mbele masuala ya uhusiano wa kimataifa na ushirikiano wa kikanda. Hii ni ishara ya dhamira ya serikali kuhakikisha Tanzania inaendelea kushirikiana na mataifa mengine kwa manufaa ya wananchi wake.

Kwa upande mwingine, Dkt. Stergomena Lawrence Tax amehamishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na sasa atashika wadhifa wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Uzoefu wake katika uongozi wa ulinzi unatarajiwa kuwa msukumo katika kuimarisha usalama wa taifa.

Tax

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *