Mbinu za NATO zafeli, Ukraine Yageukia za Kwao

Miezi kadhaa ya kusubiri kwa hamu kuanza kwa kushambulia kwa Ukraine hayakuwa ya kufurahisha kwa wanajeshi wa Ukraine ambao walifundishwa na kuwezeshwa na Marekani na washirika wake

Wakiwa na silaha za kisasa za Kimarekani kwa  mashambulizi makubwa, wanajeshi hao walikwama katika mashamba makubwa ya mitego ya mabomu ya Kirusi chini ya mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa mizinga na helikopta za kivita. Vikosi vilipotea njia. Kikosi kimoja kiliakhirisha shambulio usiku hadi mapambazuko, kupoteza faida yake. Kingine kilishindwa vibaya sana hivi kwamba maafisa walikiondoa kabisa kutoka uwanja wa mapambano.

Sasa vikosi vya Ukraine vilivyofundishwa na nchi za Magharibi vinajaribu kubadilisha mwelekeo, wanasema maafisa wa Marekani na wachambuzi huru. Wakuu wa kijeshi wa Ukraine wamebadilisha mbinu, wakilenga kuchosha vikosi vya Urusi kwa kutumia mizinga na makombora ya masafa marefu badala ya kuingia kwenye mashamba ya mitego chini ya mashambulizi. Ongezeko la wanajeshi linaendelea katika eneo la kusini ya nchi, na wimbi la pili la vikosi vilivyofundishwa na nchi za Magharibi vinafanya mashambulizi madogo madogo zaidi ili kupenya kwenye mistari ya Urusi.

Uamuzi wa Ukraine kubadilisha mbinu ni ishara wazi kuwa matumaini ya NATO ya maendeleo makubwa yanayofanywa na vikosi vya Ukraine vilivyopewa silaha mpya, mafunzo mapya, na risasi za mizinga zimefeli, angalau kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *