Maafisa wa Polisi bandia waiba shilingi milioni 72 Kutoka G4S

Wezi waliojifanya kama afisa wa polisi Alhamisi waliripotiwa kuiba shilingi 72 milioni kutoka kwa wafanyikazi wa G4S jijini Nairobi.

Kulingana na ripoti, wezi hao pia walipora pesa kutoka kwa mashine ya ATM ya Benki ya Standard Chartered jijini Nairobi Magharibi.

Habari hiyo bado inatukujia kwenye chumba chetu na maelezo zaidi yatafuata..

Hii sio mara ya kwanza pesa kupotea chini kwa namna ya sintofahamu kama hii.

Mnamo Aprili 2019, Benki ya Barclays ya Kenya ilipoteza pesa nyingi baada ya mashine zake nne za ATM kuvunjwa jijini Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *