Jamaa anunua sehemu ya matangazo ya gazeti kumuandikia Sonko ujumbe

Image result for mike sonko

Mambo yanazidi kunoga jijini Nairobi na Jumatano asubuhi, Mkazi wa Nairobi, Philip Sagoti, alinunua nafasi ya matangazo kwenye Daily Nation na akaandika barua ya kumuuomba Gavana wa Nairobi, Mike Mbuvi Sonko, kumpa kazi.

Katika barua hiyo, Sagoti alisema kwamba alikuwa mhitimu wa chuo kikuu na mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika utumishi wa umma.

Mheshimiwa Sonko nimekuandikia wazi kwa sababu sina uhakika kama mawasiliano yangu ya mapema yalikufikia. Ninajua pia kuwa unathamini uwazi.

“Ninachochewa na imani kubwa kuwa ninaweza kutoa mchango mkubwa kwa juhudi zako kuboresha jiji la Nairobi, “Philip aliongezea.

Pia aliapa kwamba atafikia matarajio ya wakaazi wa Nairobi ikiwa atapewa fursa hiyo.

“Natarajia utazingatia ujumbe huu kunifanya niwe sehemu ya uongozi katika kaunti ya Nairobi, “alimaliza.

Kiti cha naibu Gavana wa Nairobi kiliachwa wazi Januari 2018, baada ya Polycarp Igathe kujiuzulu miezi minne baada ya kuapishwa.

Igathe alidai kuwa alishindwa kupata imani ya gavana katika kuendesha majukumu ya usimamizi wa kaunti ya Nairobi.

Mnamo Aprili 2019, Gavana wa Nairobi alipoitwa na Seneti kuelezea ni kwanini hakuwa na naibu, alitangaza kwamba haikuwa suala.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *