Malalamiko baada ya Safaricom kutishia kufuta nambari za wateja waliohusika ‘kuiba’ data

Image result for safaricom company

Siku ya Ijumaa iliwakuta Wakenya kwa sehemu ‘nzuri’ na kupelekea karibu kuangusha kampuni jitu ya mawasiliano baada ya kuvuja kwa Platinum Data Plan.

Hii ilifanya wateja wengi kujinyakulia tuzo za bundles cha takriban elfu kumi na salio ya kuongea ya dakika 1500 kwa asubuhi huo.

Wateja walibonyeza *544# na kuchagua 6 ambacho kiliwafanya kununua data kutumia pointi za Bonga. Kama taarifa kwenye mitadao ya kijamii ni ya uhakika, basi kampuni ilipata hasara kubwa kwa ‘wizi’ huo.

 

Lakini sio kila mtu alinufaika na ‘wizi’ huo huku kampuni ilipojua makosa yake ikafunga sehemu hiyo ya matumizi kwa wateja wake

Cha kushangaza ni kuwa kwenye asubuhi wa kuamkia Jumamosi, kampuni ya Safaricom ilituma ujumbe mfupi kwa wateja walionufaika kwenye makosa hiyo ikiwatishia kufunga laini zao kama hawataweka salio ya angalau shilingi tano.

“Mteja mpendwa, laini yako unakaribia kufutwa kwenye mtandao. Usiruhusu hii kutokea. Weka salio ya Ksh 5 au zaidi ili kuifungua. “Inasoma ujumbe ambao Safaricom ilituma kwa wateja wake.

Image

 

Hata hiyo sehemu ya wateja inasema kuwa labda kampuni ilifanya makosa maksudi ili wapore pesa kwa wateja.

Wateja wengine waliojawa na hasira walitishia kuihama kampuni hiyo na kujisajili na Airtel au Telkom ikiendelea kutumia vitisho.

Hata hivyo, baada ya malumbano kwenye Twitter, Safaricom ilituma ujumbe mwingine wa kuomba msamaha kwa kutuma ujumbe wa kwanza kimakosa.

Image

Wengi wanaamini kuwa tangu Safaricom ianze kutumia neno ‘Oya Oya’ kwenye ujumbe mfupi badala ya ‘Dear Customer’, wateja wameipeleka kampuni na ‘Rieng’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *