Rich Mavoko aapa kamwe hataomba msamaha kwa WCB

Image result for rich mavoko

Baada ya kuondoka kwake Rich Mavoko kwenye Wasafi Classic Baby (WCB) amesema kuwa hawezi kuomba msamaha kwa bosi wake wa zamani Diamond Platinumz.

Baada ya kuondoka WCB bila neno, Rich Mavoko amekiwka wazi kuwa hamna mtu yeyote katika lebo au rekodi yoyote anayemdai msamaha.

Related image

Rich Mavoko alikuwa na mahojiano ya moja kwa moja na Dosen Selection ambapo alifunguka na mambo yaliyomwandama pale WCB.

“nilipofika WCB, sikupata msanii yeyote ambaye alikuwa amefanikiwa kimziki isipokuwa mwenye lebo mwenyewe. Sasa naomba msamaha wa nini, nilifanya makosa gani? Sina doa na mtu yeyote WCB,” alikiri Mavoko.

Image result for rich mavoko

Aliongezakuwa alikatisha mkataba baada ya mambo kwenda mrama kati yake na usimamizi wake wa zamani.

“Kandarasi yangu haikuisha. Kuna vitu ambavyo havikunipendeza na vilienda kinyume na nilivyotaka. Nilibki mda mkubwa na nyimbo ambazo sikupata nafasi kuzitoa. Kuna wakati mama yangu aliwapigia kuuliza nyimbo zangu. Sikuona siku za usoni na wao.”

Rich Mavoko alibuni lebo yake ya Billionea kid ambayo imekuja kwa kasi na wimbo wake mpya wa ‘Usizuge’ kusababisha majanga kwa maredio na vilabu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *