Mtangazaji wa Milele FM Alex Mwakideu ametuma ujumbe wa shukrani kwa rafiki zake na familia baada ya kuzikwa kwa mama yake.
Mtangazaji huyo pia alitangaza kurudi kwake kwenye redio baada ya mapumziko mafupi alichukua kufuatia msiba uliowakumba.
Alex Mwakideu alimpoteza mama yake mwezi jana na akazikwa wikendi iliyopita.
Msiba huu wa kutamausha iliakuta kina Alex na familia yake miezi chache baada ya kumpoteza dadake Emmy Mwakideu aliyeugua saratani.
Kupitia kwa mtandao wa kijamii, Alex Mwakideu aliwashukuru marafiki na jamaa waliotuma rambirambi zao, kusaidia kuchanga pesa na pia kwa maombi kwa wakati huu mgumu.
“Natamani kungekuwa na fursa ya kuandika kwa kila mmoja wenu, au hata kukumbatia kila mmoja wenu (hahaha) lakini kwa sababu siwezi kufanya hivyo sasa, nataka tu kukuahidi kuwa nitawaombea, nitamshukuru Mungu kwa ajili yenu daima,” alidokeza Mwakideu.
View this post on Instagram
Mwakideu aliongeza kuwa amejifunza mengi kutokana na msiba huu na kwa zaidi alipata kuona upendo kutoka kwa watu.
Baada ya kumuaga mama, amerudi rasmi kwa redio na maisha itaendelea.
“Sasa maisha lazima iendelee na ninaamini hata mama anataka maisha yetu kuendelea,” alisema.