Yanga kushusha ‘mashine’ ya Kinyarwanda

Inaelezwa kuwa kocha mkuu wa klab ya Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera yuko katika mipango ya kuwania saini ya kiungo hatari wa pembeni kutoka klabu ya Klabu ya Mukura Victory Sports ya nchini Rwanda, Patrick Sibomana.

Taarifa zinadai kwamba usiku wa kuamkia jana nyota huyo alipanda ndege ya RwandAir na kutua nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Yanga tayari kwaajili ya kuingia kandarasi baina ya pande hio mbili.

Mara kadhaa Mwinyi Zahera amewahi kunukuliwa akisema kuwa yupo katika mazungumzo na takribani wachezaji sita wa kimataifa ambao anawania saini zao kwaajili ya kujiunga na klabu yake. Mataifa hayo ni Rwanda, Nigeria, Ivory Coast na Guinea.

Zahera anafanya hivyo kwaajili ya kuimarisha zaidi kikosi chake kwaajili ya kutoa changamoto kubwa ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Ligi msimu ujao kufuatia hali isiyoridhisha ya msimu huu unaomalizika abapo mpaka sasa Yanga hawatakuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao kutokana na kukosa ubingwa wa TPL pamoja na kutupwa nje katika mashindao ya Kombe la Azam Sports Federation Cup ambalo hutoa mwakilishi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Championi Jumatatu, winga huyo anakuja kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kupewa mkataba wa kuichezea timu hiyo.

“Muda mrefu Yanga walikuwa wanamuwania winga huyo tangu msimu uliopita, baada ya kushindikana kukamilisha usajili wake.

“Lakini msimu huu wamepanga kumsajili katika kukamilisha ripoti ya kocha aliyoitoa ya kukamilisha usajili wa kila mchezaji anayemuhitaji katika kuelekea msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela, alipotafutwa kuzungumzia hilo, amesema: “Siwezi kukubali au kukataa ujio wa winga huyo, ukweli wapo wachezaji wengi wanaotarajiwa kutua nchini kwa ajili ya kusajiliwa, hivyo tusubirie suala hilo kama likikamilika tutaweza wazi.”

Inaelezwa kuwa jana jioni winga alionekana akiwa hoteli moja jijini Dar es Salaamna viongozi wa Yanga akiwemo Mwakalebela na Samuel Lukumay wakifanya mazungumzo ya kumpa mkataba ambao unaaminika ni wa miaka miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *