Mwana FA, Roma Mkatoliki warusha jiwe gizani suala la ufuturishaji

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA amerusha jiwe gizani kwa kusema kwamba kuna watu wana shida za kweli ambao ndiyo hasa wanahitaji kufuturishwa na kuonya kuwa watu wanaweza kukosa fadhila za Mungu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, msanii huyo ambaye ni moja ya wasanii wakongwe na bora wa kuchana amesema kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya tafrija za kufuturisha watu kama mtindo tu.

Miaka ya hivi karibuni katika nyakati tofauti tofauti za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, watu mashuhuri, wanasiasa pamoja na wasanii hususan wa muziki wamekuwa wakiandaa tafrija mbalimbali kwaajili ya kufuturisha makundi ya watu tofauti.

Hali hiyo imekuwa ikizua sintofahamu mbalimbali kwani wengi wao wanaoalikwa ni watu wenye uwezo wa kupata futari hiyo kwa uwezo wao badala ya kualikwa watu wenye uhitaji wa kweli wa jambo hilo adhimu kabisa.

Msanii mwingine wa Hip hop Roma Mkatoliki pia amekosoa dhahiri shahiri jambo hilo ambapo kupitia Twitter yake rasmi ameandika “Inashangaza Unaalika Wa2 Ftari Hata Hawakufunga,Unawaalika Tu Sababu Unajua Wana Followers So Wakipost Watu Wataona! Alika Masikini/Wasiojiweza/WenyeUhitaji Watashukuru Na Kukuombea Dua! Sisi Ukitualika Tunakuja Tunakula Tunapiga Selfie Tunasepa!Hata Asante Yetu Sio Ya Dhati.”Roma Mkatoliki

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *