Msanii wa injili Kizo B atishia kujitia kitanzi

Image result for kizo b

Msanii wa injili Kizo B amewashtua mashabiki wake baada ya kuweka kwenye mtandaoni kwamba anataka kujitia kitanzi.

Kizo B amewaaga mashabiki wake akielezea kwamba hamna haja ya kuishi tena kwa kipindi hiki ambacho kimeonekana kuwa na ugumu mwingi.

Image result for kizo b

Wasanii mara kwa mara tunawaona wakitembea na magari makubwa mpaka ata aina ya V8tunafikiria maisha yao yako shwari lakini hilo si la kutegemea.

Watu mashuhuri huwa wanapitia changamoto tele kama tu binadamu wa kawaida ila wanakuwa na ugumu wa kuelezea masuala wanazopitia.

Image result for kizo b

Kizo B alianza kama msanii wa dunia na alipitia changamoto nyingi kilichomfanya baadaye akabadili kuingia injili.

Kizo B ni mmoja wa watangulizi wa Bongo Fleva hapa Kenya na amekulia mji wa Mombasa. Hata hivyo, mziki wake wa injili haujakita mizizi kwenye sanaa ya injili nchini.

Image result for kizo b

Wimbo wake uliomtambulisha kwa wokovu ni ‘Kaa na Mungu’ aliyomshirikisha msanii wa kike, Sharon.

Lakini mbona kutaka kujiua?

Kama msanii yeyote anayekuwa hajatokea ama mziki wake kushika kasi, kuna kukata tamaa na changapmoto za mziki pia.

“Kifo ni suluhisho pekee la hali yangu kwa sasa. mwombeeni mtoto wangu awe na nguvu na nina masikitiko sana kwa Timu yangu VEKTA KENYA wewe ni bosi bora niliyekuwa nayo.” alieleza kwenye mtandao wa Facebook.

Aliendelea kuelezea mashabiki wake jinsi alivyo sikitika kuwaacha na kuwaomba wawasaidie mwana wake kwa chochote atakacho taka miaka ya kujiendeleza yakimfikia.

Tulijaribu kumfikia Kizo B lakini dua zetu hazikufua dafu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *