DRC Congo, Boti za kizamani kuzuiwa

 

 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imezuia boti za kizamani kufanya safari zake katika ziwa Mai-Ndombe kufuatia ajali iliyotokea jumamosi na kusabisha vifo vya watu 45 katika ziwa hilo huku mamia wengine wakihofiwa kuzama.

Jumatatu Gavana wa Jimbo la Bandundu nchini humo ndugu Antonie Masamba alitangaza katika kipindi cha radio kwamba boti hizo ambazo zina zaidi ya miaka mitano zitazuiliwa.

Ajali ya boti illiyotokea Jumamosi, ilihusisha boti ya mbao ambayo ilibeba watu kupita uwezo wake.  Gavana amesema, boti hiyo ilibeba abiria 400 ambao kati yao 45 wamepoteza maisha, zaidi ya 180 wameokolewa huku 200 wengine wakiwa hawajulikani walipo

Aidha, ripoti inaonyesha boti hiyo ilibeba abiria 130 huku uwezo wake ukiwa ni kubeba abiria 80.

Ajali za boti zimekua zikitokea mara kwa mara nchini DRC licha ya kua Usafiri wa boti kutumika sana kuunganisha maeneo kadhaa ambayo ni vigumu kufikika barabara nchini humo.

Mwezi uliopita watu 167 walipoteza maisha kwenye ajali mbili za majini kwenye nchi hiyo hali iliyomlazimu Rais wa DRC Felix Tshisekedi kuamrisha kuwa abiria wote wa vyombo vya majini nchini humo wavalishwe maboya muda wote wa safari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *