Mwinyi Zahera bado amganda Mkude

Hiki ni kipindi ambacho macho na masikio ya mashabiki na wapenzi wa soka la Bongo hususan wa vilabu vya Simba na Yanga yameegemea katika pilika pilika za usajili.

Kila kinachosemwa na ama makocha au viongozi wa timu zao huleta taharuki kubwa. Sasa kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hana mashaka na uwezo wa mchezaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Simba hivyo akimpata lazima amkamate kwelikweli.

Mkude mkataba wake na Simba unamalizika msimu huu na bado hajasaini mkataba mpya imekuwa ikielezwa kwamba yupo kwenye mahesabu ya viongozi wa Yanga.

‘”Mkude ni mchezaji mzuri nimemuona na nimemfuatilia kwenye mechi nyingi hivyo nakubali uwezo wake, kuhusu kumsajili hilo siwezi kusema kwa kuwa sijajua kama yumo kwenye hesabu zangu lakini nikimpata lazima nimkamate kwa kuwa anajua mpira.

“Mchezaji mzuri ni yule ambaye anaweza kukaa na mpira na kuutoa kwa muda sahihi sio kuupoteza bila nidhamu, yeye namuona namna anavyokaba na kugawa mipira yupo vizuri,” amesema Zahera.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *