Babu wa Loliondo aibuka, aitabiria mazito Tanzania

Jina la Babu wa Loliondo ni moja ya majina ambavyo yalipata kuvuma sana miaka kadhaa iliyopita kutokana na matibabu yake kwa njia ya mitishamba anayowapa watu kunywa kupitia kikombe, huduma ambayo ilikuwa ikipatikana Kijiji cha Samunge.

Ni Takribani miaka 9 tangu  kupungua kwa idadi ya watu waliokuwa wakifika katika kijiji cha Samunge, tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha kupata kikombe cha Babu, mchungaji aliyekuwa akitoa huduma hiyo Ambilikile Mwaisapile ameibuka tena na kutoa utabiri mpya.

Mchungaji Mwasapile amesema kwamba Tanzania inaenda kuwa kioo na taifa la mfano ambapo mataifa mengi kote duniani yatafika hapa nchini kujifunza mambo mbalimbali.

Akizungumzia kupungua kwa idadi ya watu wanaofikia kupata kikombe Mchungaji Ambilikile amesema kunachangiwa na uvumi uliopo kuwa Babu wa loliondo alishafariki huku baadhi ya watu wakionekana bado wakiendelea kufurahia huduma ya kikombe.

Ikumbukwe kwamba kati ya mwaka 2010 na mwaka 2011 huduma ya kikombe cha babu ilivuta maelfu ya watu kutoka kila kona ya nchi kwa kile kilicho aminika kutibu maradhi sugu ya mwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *