Robert Kidiaba alamba shavu serikali ya DRC, ateuliwa kuwa Waziri

Kipa wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya DRC na klabu ya TP Mazembe Robert Kidiaba, amechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la mkoa wa Katanga.

Kidiaba ambaye siku zake alipata umaarufu mkubwa kwa kucheza kwa makalio na kuwafurahisha mashabiki, sasa anakuwa mwanasiasa.

Wakati akicheza soka, Kidiaba mwenye umri wa miaka 42, aliichea timu ya taifa mara 61, tangu mwaka 2002 hadi 2015 lakini pia amekuwa katika klabu ya TP Mazembe, ambako hadi kuchaguliwa kwake katika bunge la nchi yake amekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo.

TP Mazembe aliyoichezea kwa muda wa miaka 14 toka alipoamua kujiunga na timu hiyo 2002 akitokea AS Saint Luc.

Kidiaba alistaafu kucheza soka 2016 na alikuwa kipa wa timu ya taifa ya Congo ila kuchaguliwa kwake kuwa waziri wa michezo wa Congo kunaweza kumfanya akaachana na kazi yake ya ukocha.

Alianza kuonesha dalili za kuwa mwanasiasa mwaka 2015, baada ya kustaafu kucheza soka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *