Kiwanda cha kuunda mavazi ya polisi Kitui ni pigo kubwa kwa ‘cartels’

Image result for Matiang'i in Kitui to Inspect Police Uniforms Making Industry

Waziri wa usalama wa ndani Daktari Fred Matiang’i Jumatano hii ametembelea Kaunti ya Kitui kwa nia ya kukagua kiwanda cha kutengeneza nguo (KICOTEC) ambayo ilipewa mamlaka ya utengenezaji wa mavazi ya polisi.

Image result for Matiang'i in Kitui to Inspect Police Uniforms Making Industry

Waziri Matiang’i aliandamana na waziri Sicily Kariuki. Wawili hao walipokelewa na Gavana wa Kitui Charity Ngilu. Hapo awali, Ngilu alitoa uhakika kuwa kiwanda cha KICOTEC kina uwezo wa kutengeneza nguo za polisi.

Akiongea kwa avyombo vya habari kwenye ziara hiyo, Gavana alisema kuwa serikali yake ya kaunti na watu wa Kitui wanashukuru rais Uhuru Kenyatta kwa fursa hii ya kuunda nguo za maafisa wa serikali.

Image result for Matiang'i in Kitui to Inspect Police Uniforms Making Industry

“Tangazo la rais la hivi majuzi inayoipa KICOTEC chanzo cha kuunda mavazi kwa machifu na wasaidizi wake ni heshima kubwa kw awatu wa Kitui kwa sababu itahakikisha kazi zimepatikana kwa vijana wetu na pia kukuza uchumi,” alisema Gavana Ngilu.

Kulingana na Matiang’i, ‘cartels’ wakubwakwa serikali walikuwa wamejitengea nafas kuziiba pesa kupitia zabuna ya uagizaji wa mavazi ya polisi. Matiang’i alisisitiza kuwa Kenya ina uwezo wa kujitengenezea mavazi zake.

Image result for Matiang'i in Kitui to Inspect Police Uniforms Making Industry

“KICOTEC ina uwezo wa kutengeneza vitengo 5000 kwa siku moja, ikipatia ajira vijana wanaozidi 400 wa Kitui ambao tumewafundisha na kuwakuza kufanya kazi kwa kiwanda hiki,” alisisitiza Ngilu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *