Nilitaka kuokoa vijana wasio na kazi, asema Brian Bera

Image result for brian bera
Picha: Kwa Hisani

Brian Bera, mwanafunzi wa JKUAT ambaye alijaribu sana kuingia katika ikulu amejitokeza kortini akisema alitaka kuokoa vijana wengi wasio na kazi nchini Kenya.

Bera mnamo Juni alipigwa risasi na maafisa wa polisi wanaolinda ikulu pale alipojaribu kuinga ndani kupitia kwa ukuta.

Aliiambia korti kuwa alikuwa mtu mzima na baba yake anapaswa kuzuiliwa kuingilia maisha yake kwani ana miaka 25.

Image result for brian bera

Bera alisema anataka mahakama imsamehe na aachiliwe huru.

Walakini, mahakama iliamuru kwamba bado atashikiliwa katika kituo cha wazimu, chini ya uangalizi wa baba yake.

Brian Bera atakuwa chini ya matibabu kwa muda wa miezi mbili na atafikishwa kortini mnamo Oktoba 9.

Mwezi uliopita, Bera aliomba Rais msamaha na korti akiahidi kutorudia matendo yake.

Kabla ya jaribio lake la kuingia katika ikulu, hapo awali alikuwa ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa angetekeleza kitendo hicho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *