Gavana Sonko Azindua Vituo vya Upimaji Saratani

Image result for sonko in mbagathi hospital

Gavana Mike Mbuvi Sonko, Jumatatu ya leo alizindua operesheni ya uchunguzi wa saratani ya bure ndani ya jiji la Nairobi.

Gavana huyo aliweka katika ukurasa wake wa Facebook kuwaarifu wakazi walioko ndani ya mji mkuu juu ya vituo ambavyo wanaweza kupata huduma hiyo ya bure.

Zoezi hilo litaendeshwa kwa wiki nzima katika hospitali za Mama Lucy na Mbagathi mtawaliwa

Sonko pia aliwahakikishia wakazi wa Nairobi wanaoishi katika makazi yasiyokuwa rasmi kuwa mipango inaendelea kuhakikisha kuwa watajumuihwa kwa Bima ya taifa (NHIF).

Alitoa hotuba zake za hivi punde alipokuwa akitembelea hospitali, kuthibitisha kama ziko tayari ili kutekeleza mpango huo.

Image result for mama lucy kibaki hospital

Katika video iliyowekwa kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook unaozingatia ziara yake, mmoja wa wauguzi alithibitisha kwamba wana uwezo wa kushughulikia zoezi hilo, kwani walikuwa na mashine muhimu.

Harakati mpya ya kupambana na saratani inakuja baada ya mwezi wa giza kwa Kenya, ambapo viongozi wake 3 tajika- Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom, Bob Collymore, Mbunge wa Kibra, Ken Okoth na Gavana wa Bomet, Joyce Laboso – kuaga dunia kwa ugonjwa huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *