Uasingishu ipo tayari kumpokea rais Uhuru Kenyatta

Image result for uhuru kenyatta

Maandalizi ya kuanzishwa kwa kiwanda cha nguo cha Rivatex huko Eldoret ambayo itaongozwa na rais Kenyatta Ijumaa wa leo yalikuwa katika mbwembwe Alhamisi jioni, huku wakitupilia mbali tahadhari ya tofauti kati ya rais na naibu wake William Ruto ambaye ni mkaazi wa kaunti hiyo.

Baadhi ya wakosoaji wa Rais kutoka kaunti ya Uasin Gishu, ambayo ni nyumbani mwa Ruto walikiri kuwa hawakuwa na tatizo la kumpokea Mkuu wa Nchi.

Rais anatarajia kushuhudia hafla hiyo ya kuzindua vifaa vya kisasa kwenye kinu cha nguo wakati wa ziara yake ya kwanza kwa kanda mwaka wa 2019.

Image result for uhuru kenyatta

Oscar Sudi na mwenzake wa Soy Caleb Kositany ambao ni washirika wa karibu wa naibu rais, walisema kazi hiyo si tukio la kisiasa, na kupuuzilia mbali madai ya kuwa dhidi ya ziara hiyo.

“Tunataka kukushukuru rais kwa kuunga mkono kituo hicho. Kama viongozi, tunasema kuwa tunaweza kutofautiana kisiasa, lakini wakati wa maendeleo, tunaweka tofauti hizo mbali, “Bw. Sudi alisema.

Related image

Sudi na mwenzake Kositany waliwahimiza wakaazi kujitokeza kwa wingi kumpokoea rais Uhuru Kenyatta kwa uzinduzi huo.

Itakumbukwa kuwa hao viongozi wawili wamekuwa mstari wa mbele kupinga hndisheki kati ya Raila na Uhuru wakisema kuwa ilikuwa kuharibu mpango wa Ruto kuwa rais mwaka wa 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *