Jinsi ya Kudhibiti na Kuepuka Kisukari na Homa ya Ini

Tupate elimu kidogo kuhusu KISUKARI

Huu ni ugonjwa wa kudumu ambao unaathiri jinsi mwili unavyochakata glukosi.

Ulaji usiofaa, kutofanya mazoezi na vinasaba huweza kuongeza hatari yako ya kupata kisukari

Dalili za kisukari zinajumuisha: Kiu kikali mara kwa mara, Kukojoa sana, uchovu, njaa mara kwa mara na zingine.

Kuzuia kisukari unahitaji kubadili mitindo ya maisha ikiwemo kuboresha ulaji wako (kula kwa nidhamu), kufanya mazoezi, kudhibiti uzito huweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kisukari.

Iwapo tayari una kisukari, ili kudhibiti sukari hakikisha unafuatilia sukari yako ya kila siku, unatumia dawa kama ulivyoelekezwa unazingatia mitindo bora ya maisha kwa watu wenye kisukari.

Tambua, sukari isipodhibitiwa madhara ni makubwa hasa ugonjwa wa moyo, figo, upofu na kuharibu mishipa ya fahamu.

Kundi la maradhi yanaoathiri INI na huweza kupelekea ini kuharibika na kushindwa kufanya kazi.

 

Sababu kuu za ugonjwa wa Ini ni uywaji wa pombe, maambukizi ya virusi hasa vya hepatitis B na C na ugonjwa wa ini kujaa mafuta.

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa Ini ni uchovu, tumbo kuuma manjano hasa machoni a zinginezo.

Boresha Afya ya Ini kwa kudhibiti pombe, kushiriki ngono salama, kupata chanjo dhidi ya Hepatitis B na lishe bora

Chanzo; Dr. Norman Jonas tweets.

https://mobile.twitter.com/NormanJonasMD

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *